Mara nyingi jamii za wafugaji hupuuzwa kanakwamba si wadau muhimu katika bayoanuai ya Afrika. Licha ya matishio mbalimbali wanayoyapitia kama vile-kuzuiwa njia za kupitisha mifugo, vurugu, na uhaba wa shule na huduma za afya – ila aina ya mifumo ya chakula walioyoitumia imesalia kuwa aina madhubuti ya kilimo katika maeneo kavu waishiyo. Kama ardhi na nyasi ziliwazo na mifugo yao hazitabinafishwa.Hali-mbaya kama hii inatishia jamii za wafugaji za Maasai na Kalenjin waishio jimbo la Bonde La Ufa nchini Kenya. Wamaasai na wakalenjin wapo katika mapambano ya kumzuia mtu binafsi kutwaa haki-hodhi juu ya aina mbalimbali za nyasi za buffel ambazo jamii imezitumia kwaajili ya mifugo yao kwa zama nyingi. Hali inasadifu namna Haki ya Wazalishaji Mimea (Plant Breeders Rights), ambayo ni aina ya haki miliki kwenye mimea, itakavyoathiri wazalishaji chakula wa kiafrika na ni kwanini bara zima linapaswa kupinga vikali ubinafsishaji wa bayoanuai.Umuhimu wa nyasi za buffel kwa wafugaji nchini KenyaGeofrey Letakaan ni mzee wa miaka 63 wa kikalenjin, jamii ya asili ya wafugaji iishio kaunti ya Baringo, Kenya.“Nyasi za buffel zimekuwepo tangu zama za baba yangu, babu yangu mpaka zama za baba wa babu yangu,” anasema Letakaan. “Nyasi hizi zina thamani kubwa.Walishwapo ng’ombe hunenepa katika kipindi cha miezi mitatu. Zipo nyasi kwaajil ya kuunda marobota ya nyasi zinazohifadhiwa kwaajili kulishia mifugo yakiwa katika umbo la mviringo ama mraba (hay for baling), na zinatumika pia kwaajili ya kuezeka. Zamani, wazee walikuwa wakisema ‘nangrongong’, wakimaanisha ‘zipo (nyasi za buffel) katika vilima’ kama vile vilima vya Arabal na Mukutani……Watu wanapaswa kupanda nyasi hizi- wote.”Mtazamo wa Letakaan ni kama mwangwi wa mitazamo ya wengi katika kaunti ya Baringo, uwanda wa nyasi ndani ya jimbo la Bonda La Ufa nchini Kenya. Katika kaunti hiyo pia wapo jamii ya Ilchamus ambayo ni sehemu ya jamii kubwa ya Maasai. Wakalenjin na wailchamus ni wafugaji wategemeao ng’ombe wao na mifugo mingine.Wafugaji wa Baringo husifika kwa upandaji wa nyasi za African foxtail (kisayansi huitwa Cenchrus ciliaris), kwa umashuhuri huitwa “nyasi za buffel”. Tangu kale, wanajamii wamekuwa wakilisha mifugo yako nyasi hizi. Watu wa Ilchamus huziita nyasi hizi “Lhomer aingok” na watuge, amabo ni sehemu ya wakalenjin, huziita “Lhomer Kwan”. Huzitumia nyasi hizi kama suluhu ya muda mrefu kwasababu zimeweza kuhimili aina mbalimbali za udongo, hujanua hata katika mvua chache na zimesifika kama nyasi zenye uwezo mkubwa wa kustahimili ukame.Huko Baringo na maeneo mengine ya Kenya yanye ardhi iliyo kame na nusu kame, nyasi za buffel ni muhimu mno na zenye ufanisi katika matumizi yake. Licha ya kuzitumia kama chanzo cha lishe, jamii pia zime marobota ya nyasi kwaajili ya kuuza na kuhifadhi kwaajili ya kulishia mifugo katika kipindi cha ukame. Zikiwa na kiwango kingi cha protini cha asilimia 12, nyasi hizi hunenepesha haraka mifugo. Baadhi ya wanajamii wamekuwa wakijihusisha na biashara ya kununua mifugo kwa bei ndogo, kisha kuinenenpesha kwa virutubisho vya mlo wa nyasi za buffel, na kuiuza kwa bei ya juu baada ya miezi mitatu. Pia, mbegu za nyasi hizi huwa na bei ya juu sokoni, kuanzia Ksh 300(US$ 3) mpaka Ksh 750(US$ 7.5) kwa kilogramu.Wanawake ndio huwajibika katika kulisha mifugo katika jamii za wafugaji, ilhali wanaume wakisimamia machungo/malisho. Hivyo wanawake, hutegemea kwa kiasi kikubwa kuunda malobota na kuhifadhi nyasi za buffel, hususani katika kulisha mifugo midogo (ndama) nyakati za kiangazi, wakati majani yakiwa machache.“Ninakwenda tu katika ghala, na kuchukua lobota na kuwalisha ndama wa ng’ombe na mbuzi,” anasema Shalline Parkolwa, mwenye miaka 29. Anatambua kuwa ndama wakilishwa vema, hawatohitaji kunyonya sana. Hivyo maziwa mengi yatapatikana kwaajili ya familia, hivyo hivyo kuathiri kwa uchanya juu ya hali ya lishe na uhuru wa chakula, hususani kwa watoto na wazee. Kwa ziada, wanaume wanapojenga nyumba, wanawake hupewa jukumu la kusaka nyasi za kuezeka. Nyasi za buffel ni nzuri kwa kuezekea kwasababu mirija yake ni mirefu na imara. Wanawake pia wanaweza kujipatia kipato kwaajili yao binafsi na kukimu mahitaji ya kaya zao kwa kuuza mbegu za nyasi za buffel.Anaingia Murray RobertsKwa iongo michche iliyopita, mtu aitwaye Murray Roberts, akifahamika kwa wenyeji kama “Omari” amekuwa akiongoza jitihada za kujaribu kubadili uratibu wa asili(wa wenyeji) wa nyasi za buffel – kutoka katika mfumo wa umilikaji wa pamoja wa ardhi na ufugaji kuwa katika mfumo wa kibinafsi wa umilikaji wa ardhi na kilimo makini.Robert Murray, director of RAE, and staff in the Baringo company store on February 17, 2021. Photo: Seed Savers Network (SSN)Roberts ni raia wa Kenya ambaye anatokana na walowezi wa kizungu waliopata ardhi eneo la Baringo nyakati za utwaaji ardhi kwa hila wa ukoloni wa maingereza, waliotengeneza biashara kubwa kubwa za familia zao kwenye mashamba, maeneo ya hifadhi na safari za utalii. Mwaka 1982, Roberts aliasisi taasisi ya uhifadhi iitwayo, Rehabilitation of Arid Enviroment (RAE) Trust, ili “kubadili maeneo kavu yenye mmomonyoko kuwa tambarare zenye faida kwa maslahi ya watu na mazingira”. Taasis RAE imekuwa ikijaribu kufanya hayo kwa kudahili wanajamii wenyeji kwenye mipango ya wazalishaji wa uzalishaji wa nyasi za buffel nakushawishi wazee wenyeji kuimegea mapande ya ardhi kwaajili ya taasisi hiyo kulima. Kwa maneno ya Roberts mwenyewe:“Tulianza hapa mwaka1982, kwanza kabisa kwa sababu ya mfadhili, ndiyo tuliruhusiwa kushughulika na jamii, hivyo tunayo maeneo mengi ya jamii hapa na kisha, mfadhili alipobadilika, tuliweza kwenda kwa watu binafsi. Kwakuwa sasa tumepanda katika maeneo ambayo watu binafsi walikuwa na meneo ambayo ambayo hupanda mahindi, tulianza kupanda nyasi katika maeneo hayo. Mshirika wangu ndiye aliyekuja na wazo hilo. Sasa wazo lote la kupanda nyasi kibinafsi limeshika kasi. Hili suala lote la malisho limekuwa kiwanda hapa Baringo. Ni kiwanda kwa sasa. Na ngoja nikwambie, niwepo ama nisiwepo, kiwanda hiki(shughuli za uzalishaji nyasi) kitasonga meble. Hakinitegemei mimi kwa sasa. Maeneo ya pamoja, kama nisipokuwepo hapa, yatakufa kwasababu hakuna yeyote katika jamii ambaye atayazikngatia jambo la jamii. Wakitakacho ni kulisha tu. ”Wenyeji wanasema jitihada za RAE zimebadili mahusiano baina yao na nyasiza buffel. “Nyasi za buffel zimekuwepo hapa kwa miongo mingi. Kitu pekee ambacho wanajamii hawakukifahamu ni nguvu yake (nyasi za buffel) kibiashara,” anasema mwanajamii George Letakaan.Leo hii wakaazi wengi wa jamii za wenyeji wanazalisha na kuuza mbegu za nyasi za buffel.Wengine wakiuza mbegu kupitia RAE, wakati wengine wakiuza kupitia Kerio Valley Development Authority (KVDA), wakala wa serikali ya kanda. Mwanajamii mmoja, Jackson Lekombe, ambaye amechagua kutozalisha mbegu kwaajili ya RAE, anasema yeye huuza moja kwa moja kwa KVDA na kwa ushirika kupitia Nooseya Self Help Group, ambao wanachama wake 25 wanajihusisha na biashara ya malobota ya nyasi na mbegu.Uporaji mbeguJuhudi za Roberts kubinafsisha usimamizi wa mbegu za nyasi za buffel hazikukomea katika kujiepusha na jamii na badala yake kufanya kazi na mtu mmoja mmoja. Mwaka 2001, RAE ilianza programu ya uzalishajiwa mbegu za buffel. Mwaka 2012, ilifanya maombi na kupewa Shahada ya Kinga ya Uelekeo (certificate of protective direction) – aina ya haki kwa wazalishaji ya muda mfupi wakati maombi yao yakiwa kando – juu ya kuzalisha aina mbalimbali za nyasi za buffel kutoka kwa mdhibiti wa mbegu nchini Kenya, Kenyan Health Inspectorate Services (KEPHIS). Aina ya mbegu igombaniwayo, ambayo Roberts anadai ni mali yake binafsi, inaitwa Baringo 1.Kwa kupewa shahada hiyo, Baringo 1 iliongezwa katika orodha ya aina za mbegu za taifa la Kenya. Hii inamaana kwamba haiwezi kufanyiwa biashara bila idhini ya mmiliki. Mwaka 2014, Roberts alikwenda hatua ya mbali na kufanya maombi ya haki ya wazalishaji mimea (PBRs) kwa Baringo 1, akilenga kutafuta umiliki-timilifu wa mbegu kwa gharama ya haki za wakulima. Roberts anakusaidia kusajili aina nyingine tano kwenye haki za wazalishaji mimea.Chini ya Sheria ya Mbegu na Aina za Mimea ya mwaka 2012 ya nchi ya Kenya – ambayo inatokana na tolep la Mkataba Umoja wa Ulinzi wa Aina Mpya za Mimea (Union for Protection of New Plant Varieties Convention, UPOV 1991) mwaka 1991 – mzalishaji yeyote awe umma ama binafsi, mwenyeji ama mgeni anaweza kufanya maombi na kupata haki-hodhi juu ya aina mpya ya mmea waliyoigundua ama kuzalisha. Isivyo bahati hii inaweza kuhusisha, aina zinazotumiwa na wakulima. Na hapo ndipo mgogoro kuhusu nyasi za buffel za RAE unapoibuka.Kwa wafugaji wengi wenyeji, Roberts anajaribu kuleta madai ya umiliki wa bayoanuai yao. Eresia Erige, mwanajamiiwa Baringo anasema kwamba kwa kadiri jamii walivyozidi kupata uelewa kuhusu maombi ya Roberts ya haki ya uzalishaji, wazee wenyeji walikwenda milimani na kukusanya sampuli kwaajili ya kufanya ulinganifu na aina zinazozalishwa na RAE. Waligundua zilikuwa ni nyasi za aina moja. Kwa Erige, “nyasi zile ni za milima na hivyo, mbegu zake na kilimo chake kwa ujumla kinapaswa kuwa cha wote na si kubinafsishwa.”Wanafarijiwa na mtazamo unaopatika katika katiba ya Kenya, uliopitiwa upya mwaka 2010 unaosema kwamba jamii za wenyeji zitakuwa na haki ya “umiliki wa aina ya mbegu na mimea ya asili/jadi, nasaba/jeni, tabia zake tofauti na matumizi yake”. Kwa msingi wa kikatiba, jamii za Baringo zinapaswa kuwa na haki ya kijamii juu ya nyasi za Buffel. Hata hivyo, Sheria ya Mbegu na Aina za Mimea ya mwaka 2012 ina mkanganyiko wa kikatiba ambapo inaruhusu watu kama Roberts kutwaa haki binafsi juu ya nyasi za buffel. Matokeo yake, kuna mgogoro baina ya haki za wazalishaji na haki za wakulima katika Kenya.Hata Kerio Valley Development Authority pia wamepinga maombi ya Roberts ya kutaka apatiwe Haki ya Wazalishaji Mimea, PBR. Katika barua kwake (Roberts) ya mwaka 2016, KVDA ilisema kuwa imekuwa ikijaribu na kuzalisha Cenchrus ciliaris tangu mwaka 2001 na tayari ilishaziingiza nyasi kwenye mchakato wa kitaifa wa majaribio. Ilitoa hoja kuwa RAE Trust isingeweza kuzalisha aina ilizoziwasilisha kwa kuwa haikuwa hata na program ya uzalishaji wa mmea.Zaidi, KVDA ilisisitiza kuwa nyasi za buffel zinapaswa kumilikiwa na umma na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo na Mifugo ya Kenya (KALRO) ndiyo ipewe jukumu la usimamizikwaniaba ya maslahi ya umma.KALRO wanabainisha kuwa Cenchrus ciliaris ni apomiktiki. Hii ina maana kuwa inajizalisha kupitia jinsi moja kwa kupitia mbegu. Yeyote anayedai kuwa ameunda aina mpya ya mbegu za nyasi hizi atapaswa afafanue hatua za uzalishaji alizozipitia. Hadi leo, RAE wameshindwa kutoa taarifa hiyo. Ukosoaji wa kurejewa ni kuwa nyasi hizi zinamea na kukua katika kaunti nyingine ikiwemo Kilifi, Marsabit, Mandera, Kitui na Makueni. Kwa maoni KALRO, katika kiasi cha Cenchrus ciliaris lazima kunapatikana Baringo miongoni mwa nyasi tofautitofauti za aina ile kwa asilima 99.Nooseiya pastoralists/farmers from the Ilchamus community, February 11 2021. Photo: Seed Savers Network (SSN)Mwaka 2016, KEPHIS iliandaa kikao na Roberts, jamii za wenyeji, KVDA na KALRO ili kusaka maazimio rafiki juu ya mgogoro. Katika kikao, wakala mbalimbali wa umma za Kenya, ikiwamo Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, zilikataa maombi ya Murray ya kupatiwa PBRzikitamka kuwa aina tajwa alizokuwa akiziombea haki zilikuwa ni za “umma” na zilikuwa na manufaa ya kuwa za kiasili zikiwa na “maarifa ya kawaida (juu ya uzalishaji wake)”. Lakini Murray hakukubali. Alikuwa akiharibu kikao kwa kusimama na kutuhumu jamii kwa kupora “mbegu yake”. Murray alidai kuwa ni yeye pekee ndiye alikuwa na “haki ya wazalishaji” juu yanyasi za buffel, na jamii, KVDA na wazalishaji wengine wa mbegu walikuwa wakikiuka sheria.Jedwali 1: Mlolongo wa matukioKipindi/MwakaTukioHadi mwaka 1982Wafugaji wakalenjin na wamaasai walikuwa wakichunga na kulisha mifugo yao nyasi za buffel katika nyanda zao.1982Murray Roberts kupitia shirika lisilo la kiserikalila Rehabilitation of Arid Enviroment (RAE) Trust, anaanzisha programya nyasiza buffel inayowashirikisha wanajamii wenyeji wa Baringo1991Mkatraba wa UPOV unafanyiwa marekebisho huko Geneva na kuwekwa katika hali yake ya sasa1999Kenya inakuwa mwananchama wa UPOV2001Murray Roberts anaanza kuzalisha mbegu za nyasi za buffel2010Kenya inapata katiba mpya ambayo inatambua haki za jamii wenyeji juu ya mbegu zao na maarifa yao mbalimbali ya jadi.2012RAE Trust inapewa shahada ya mwelekeo wa kinga kwenye aina ya nyasi ya Buffel, shahada ilotolewa na KEPHIS2012 (Desemba)Mabadiliko ya Sheria ya Mbegu na Aina za Mimea ya mwaka 2012 ya Kenya yanapitishwa2014Mzozo baina ya jamii za Baringo, RAE Trust na KVDA juu ya maombi ya kupata Haki za Wazalishaji Mimea yaliyofanywa na RAE2016Kenya yajiunga rasmi UPOV 1991 na kuanza kuwajibika kiutimilifu kutekeleza masharti ya mkataba2017Serikali inatangaza kucapisha shahada ya misho kuipa RAE haki ya kuingiza sokoni nyasi za Buffel aina ya Baringo 1Kipi ki mashakani?Kilicho mashakani katika mgogoro huu ni haki za wakulima kuhifadhi kubadilishana na kuuza mbegu za nyasi za buffel. Ikiwa PBR itatolewa, hawataweza kuzalisha ama kuzifanyia biashara mbegu bila ruhusa ya Roberts na malipo ya mrahaba kwake. Hili litaathiri kwa uhasi moja kwa moja maisha ya wanajamii wenyeji ambao daima wamezitumia na kuzitegemea. Kwa hili la Baringo 1, jamii za wenyeji na maofisa wa umma hawaamini kama Roberts alifanya kazi ya uzalishaji kama anavyodai. Wanapinga kwa urasmi uhalali mawasilisho yake katika mamlaka za usajili na haki wazalishaji mimea.Ni muhimu kukumbuka kuwa RAE haiku peke yake katika kutafuta umiliki wa nyasi za buffel. KALRO na KVDA zote ni taasisi ambazo zina maslahi katika kupata uhodhi na biashara ya nyasi za buffel. Ugomvi baina yao unachochewa na ukweli kuwa RAE iliwapiku ujanja wengine hao wawili katika mchakato wa usajili wa aina hiyo yam mea. “KARLO pia inayo mabavu ya kuwapiku wengine. Tatizo si taasisi yeyote, lakini sheria ya mbegu itokanayo na UPOV 1991, ambapo jamii inaendelea kutaabika, bayoanuai inaendelea kuharibiwa, na haki za wakulima hazilindwi,” anasema Daniel Wanjama, Mkurugenzi wa Mtandao wa Waokoa Mbegu nchini Kenya.Hivyo hali ya kutokuwa na hakika kwa jamii mbalimbali za Baringo kunasalia kuwa juu. Maombi ya PBR ya Murray hadi sasa yanashughulikiwa kando na KVDA imechukua hatua za kisheria kuzuia jaribio ambalo ni kama halina tija. Kwa sasa Murray Roberts na RAE Trust anaendelea kuongeza na kuuza mbegu. Hata hivyo, kwasababu ya jambo hili kushika hisia za wengi, hatishii tena jamii za wenyeji kuhusu “kupanda mbegu zake”.Kwa sasa, wanajamii wa Baringo wanamekusudia kuendelea kupanda nyasi za buffel na kupuuza madai ya Murray juu ya mbegu zao. Katika safari hii, wanaungwa mkono na Wizara ya Kilimo, ambayo imejitokeza na kusema haki ya wazalishaji juu ya Baringo 1 isitolewe.Hata hivyo, hii “ni jitihada isiyo na tija na haina la ziada zaidi kujikosha kijamii kwasababu haki za wakulima tayari zilikwisha kuvunjwa wakati aina ya Baringo 1 iliposajiliwa katika Orodha ya Taifa ya Aina za Mimea,” anasema Domonic Kimani wa Mtandao wa Waokoa Mbegu.Hapana kwa RAE, hapana kwa KVDA, hapana kwa umiliki mbegu kibinafsi.Shalline Parkorwa, Nooseiya pastoralist/farmer from the Ilchamus community, showing buffel grass seeds on February 11, 2021 - Salabani village, Baringo. Photo: Seed Savers Network (SSN) Mgogoro huu unaonesha namna sheria na kanuni zinazodhibiti sekta ya mbegu zimeundwa kuyanufaisha makampuni ama watu binafsi kwa mkanganyiko wa moja kwa moja na haki za wakulima na jamii za wenyeji.Kwa hili la nyasi za buffel, Murray anatumia tu mlango tu wa ubinafsishaji mbegu unaotengenezwa na Sheria ya Mbegu na Aina za Mimea ya Mwaka 2012 ya nchi ya Kenya – itokanayo na UPOV 1991.Ilikuwa ni suala la muda tu kabla RAE hawajakimbilia katika mkondo wa sheria kudai uhodhi na udhibiti wa aina ya mmea ambao maarifa kuuhusu ni ya wote na ya kawaida. Ulinzi wa kweli wa wafugaji na wakulima wa Kenya utakuja pale Kenya itakapoitupili ambali sheria ambazo msingi wake ni UPOV. Jaribio la hivi punde la KVDA na mamlaka nyingine za umma kumzuia Murray asipate PBR lazima zionekane kwa namna zilivyo: mvutano wa ubinafsishaji mbegu. Hata kama jaribio la RAE kupata PBR lisipofaulu, wafugaji huko Baringo watapoteza haki zao kutumia, kuhifadhi na kuzalisha nyasi za Baringo 1, kutoka kwa KVDA ama yeyote mwingine. Jaribio lolote la kulinda mmea huu wa millennia tena wenye utajiri wa utofauti lazima lifanyike kupitia wadau wake wa kweli: wafugaji, wakulima na jamiii ambazo zimeitunza mimea hii kwa vizazi vingi.Rejea[1] Wakalenjini ni kundi la wakaazi-asili wapatikanao katika Kaunti ya Baringo katika jimbola Bonde la Ufa nchini Kenya.[2] AFSA (2018). Ufugaji: Uhuru wa Chakula kwa matendo. Inapatikana katika https://afsafrica.org/case-studies-pastoralism/[3] Mwanajamii ya wenyeji, aliyeshindwa kutamka vema jina lake (Murray Roberts) na kumuita “Omari”[4] Dondoo za historia ya familia hii zinafafanulia na eneo ambalo kampuni ya bwana Murray Roberts r: http://robertssafaris.com/our/history[5] Tizama: http://www.raetrust.org/[6] Tizama, "Sehemu II Mmmonyokowa Ardhi na Mitigation katika Africa,” katika Ukaguzi wa Mmomonyoko wa Ardhi Kukua kwa Jangwa, Suluhu na Uzuiaji," iliyohaririwa na Pandi Zdruli, Marcello Pagliai , Selim Kapur, Angel Faz Cano , Springer Science & Business Media, 2010, p.117.[7] Mahojiano na Mtandao wa Waokoa Mbegu, March 2020[8] Hati miliki kifungu cha pili kinaashiria kwamba mwombaji haki za ubinafsishaji lazima awe ni mtu aliyezalisha ama kugundua aina yam mea husika ama mrithi wake katika kitengo hicho. Na masharti ya sehemu ya kwanza yataadhiri ikipewa kipaumbele mhusika ambaye anazalisha ama kugundua mbegu[9] Sheria Kenya: Katiba ya Kenya, Ibara ya 11.3(b). Inapatikana http://kenyalaw.org/kl/index.php?id=398[10] Kwa kadiri ya nyaraka zilizotizamwa mna waandishi[11] Kwa kadiri ya KALRO[12] Mahojiano na Mtandao wa Waokoa Mbegu, March, 2020[13] Mahojiano na Mtandao wa Waokoa Mbege, March 2020.[14] Kwa kadiri ya nyaraka zilitizamwa na waandishi