https://grain.org/e/6284

Mazao biofuti (biofortification) au bionuwai (biodiversity)?

by GRAIN et al. | 11 Jul 2019
Mapambano ya kutafuta suluhisho haswa la utapiamlo yameanza. Jiunge na uchukue hatua!

"Biofuti" (Biofortification) inalenga kuongeza virutubisho chache katika mazao kwa njia ya kuzalisha mimea, kwa kutumia mbinu za jadi au zana mpya za bioteknolojia. Ingawa kuna virutubisho Zaidi ya 40 ambavyo tunapaswa kupata kutoka kwa chakula chetu kwa afya bora, lengo la utafiti wa biofuti ya mazao ni tatu tu: madini ya zinki, madini ya chuma na virubutisho (vitamini) A.

Utafiti bado unaendelea ili kuendeleza biofuti ya mazao ya mchele, ngano, mahindi, ndizi, ndengu, viazi vitamu, mhogo, maharage na mahindi huku Afrika, na pia Asia na Latin America. Jitihada za umma zinasi-mamiwa na Kundi la Ushauri Kuhusu Utafiti wa Kimataifa wa Kilimo (CGIAR), katika vitengo vitatu: Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Mchele (IRRI), inayozingatia mchele wa viini tete (GMO); Kituo cha Kimataifa cha Viazi (CIP), kinachozingatia viazi vitamu; na miradi ya HarvestPlus, ambayo inaratibu zingine zote. Fedha za kazi hii ya biofuti zinatoka kwa Bill Gates, USAID, na kadalika. Utafiti binafsi unafanyika pia na Pepsico, Dupont, Bayer, Nestle na wengine.

Wanaounga biofuti mkono wanadai kwamba ni njia ya gharama nafuu ya kushughulikia utapiamlo (malnutrition): baada ya kuzalisha mmea, unaweza kuupanda tena na tena. Mara nyingi waounga hutumia lugha ya udanganyifu ili kupendekeza hii mimea, kuanzia na neno “biofuti” lenyewe. Neno hili linashauri kwamba vyakula vingine vyote au mimea ingine ni dhaifu kabisa au zina upungufu.

Maneno kama “golden rice” “superbanana” na “orange maize” hutumiwa kuwashawishi watumiaji kuwa mbegu au vyakula ambavyo ni biofuti ni bora kuliko vingine vyote ambavyo sio biofuti. Majina haya, na pia mazao yenyewe, wakati mwingine husajiliwa kama haki miliki za kitaalamu, hata ingawa yanatakiwa kutumiwa bila malipo yeyote.

Hadi sasa, karibu aina 300 za mazao biofuti, zimetengenezwa na kutolewa duniani kote. Ingawa hakuna mimea iliyo na viini tete (GM) ambayo imewafikia wakulima, idadi kubwa ya mimea hiyo iko kwa mikakati ya kutolewa.

Wanawake na watoto mara nyingi, hudaiwa kuwa ni wamiliki wakuu wa mazao ya mimea biofuti. Lakini wakaaji wa vijiji na makundi ya wanawake ulimwenguni kote, mara nyingi wanaonelea yakwamba mifumo ya vyakula mbalimbali vya jadi na mlo wa jadi, ndio suluhisho halisi la umasikini na utapiamlo.

Miradi muhimu kadhaa ya utafiti wa mimea biofuti

GRAIN na marafiki wametoa wito wa kukaribisha vikundi vya wanawake na mashirika ya wakulima, ili kuchun-guza suala la biofuti katika - nchi, kanda, kitaifa au kimataifa. Tunadhani kuna maarifa na uzoefu wakutosha unoweza kuhalalisha kukataa kwa mazao na vyakula vyote biofuti, pamoja na kulazimisha uwekezaji katika utafiti wa mbinu tofauti za kilimo kulingana na agroikologia, utamaduni, na umiliki wa chakula.

Tunapendekeza kuwa mbinu mbadala za kukabiliana na njaa na utapiamlo zinawezekana kulingana na kanuni tano zifuatazo:

1. Kueneza habari na elimu kuhusu lishe bora na maisha, kwa kusisitiza usawa wa wanawake na usawa wa kijinsia;
2. Kuimarisha uongozi wa wanawake katika uamuzi wa sera za chakula na utafiti wa mifumo ya chakula;
3. Kueneza nuwai katika kilimo na katika vyakula, sio vyakula aina moja pekee. Hii inajumuisha udhamani wa mimea na wanyama asili, chakula ya kitamaduni, mbegu na elimu asili inayoimarisha afya na kuimarisha jamii;
4. Kupunguza gharama na kuongeza upatikanaji wa matunda na mboga, njia moja ikiwa ni kurejesha ruzuku na fedha nyingine za umma, ambazo kwa sasa zinatumiwa kueneza bidhaa za viwanda na vyakula duni vilivyotengenezwa; na
5. Kuzuia uriberali mamboleo wa chakula na kilimo ambao huchukulia chakula na mimea kama bidhaa ambazo wameweka milki ya utaalamu wa kisheria, ili kuwezesha makampuni haya kujifaidi wenyewe. Kushughulikia sababu haswa za umasikini na njaa yahitaji chakula na kilimo ziwe chini ya udhibiti wa umma na jamii.

Ili kujifunza zaidi, angalia taarifa kamili “Mazao biofuti au bionuwai? Mapambano ya kutafuta suluhisho haswa la utapiamlo yameanza” kwenye https:// www.grain.org/e/6246

GRAIN, Pesticide Action Network Asia Pacific (PANAP), Food Sovereignty Alliance India, People’s Coalition on Food Sovereignty (PCFS), Eastern and Southern Africa Small Scale Farmers’ Forum (ESAFF), Growth Partners Africa, Participatory Ecological Land Use Management (PELUM) Kenya, Kenya Food Alliance, Participatory Ecological Land Use Management (PELUM) Uganda and African Biodiversity Network (ABN).
Author: GRAIN et al.
Links in this article:
  • [1] https://